Luke 20:20-25

20 aKwa hiyo wakawa wanamchunguza na kutuma wapelelezi waliojifanya kuwa wenye haki ili wapate kumtega kwa maneno asemayo, ili wamtie katika uwezo na mamlaka ya mtawala. 21 bHivyo wale wapelelezi wakamuuliza, “Mwalimu, tunajua unasema na kufundisha yaliyo kweli wala humpendelei mtu, bali wafundisha njia ya Mungu katika kweli. 22Je, ni halali sisi kulipa kodi kwa Kaisari, au la?”

23Lakini Isa akatambua hila yao, kwa hiyo akawaambia, 24“Nionyesheni dinari. Je, sura hii na maandishi haya yaliyoko juu yake ni vya nani?”

25 cWakamjibu, “Ni vya Kaisari.”

Akawaambia, “Basi mpeni Kaisari kilicho cha Kaisari, naye Mungu mpeni kilicho cha Mungu.”

Copyright information for SwhKC